"CCTV Footage showing how the frama involving stolen car and witch doctors was stage managed". BY Mombasa County Government Watch's Video. Obtained online
Katika zama hizi za #Uwazi, #Ukweli, #Teknolojia na #Globalization, ni vigumu kuficha vitu vya kupotosha na nia ya kuua roho. Kwa kunukuu hii video clip hapa na utafiti kutoka kwenye mengine, mengi kuhusu #Ushirikina ni ya #Uongo na upotoshaji. Ukisikia Mtu anamtangazia mwenzie kuwa #Mchawi, mtu huyo mwenyewe ndie #MCHAWIMKUU. Hakuna #Ushahidi wala uthibitisho wa #Kisheria ao #Kisayansi.
Biblia takatifu yatuambia kuwa, Mtu mwongo, Msengenyaji, Mpotoshaji, ndie mchawi na aua roho. Uchawi ni #sanaa na #imani (Mfano Dini ya Wicca) ya kupotosha na kukandamiza wengine kwenye jamii, inayotumiwa na watu wenye nia ya kuangamiza roho kwa kuathiri mtu mwingine kisaikolojia. Uchawi hauna lolote zaidi ya upotoshaji wa mtu/watu kwenye jamii na kuzua chuki za kukithiri.
Pia, Biblia Takatifu imewafananisha WACHAWI/Washirikina na watu hawa: "wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote", UFUNUO 21:8; na tena "uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo", WAGALATIA 5:19-21.
Usiwakosoe, Biblia katika kitabu cha Mithali 9:8-9 yasema hivi: "Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. 9 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu".
Mungu azidi kutubariki wanadamu na vituko vyetu. Go Figure! πππ✡
Utafiti/Research By Mr. Masao
Nukuu zaidi: The Definition of Witchcraft In The Bible – And Should We Be Worried About It? Link: https://www.scriptureincontext.com/the-definition-of-witchcraft-in-the-bible-and-should-we-be-worried-about-it/