Saturday, September 16, 2017

Uchawi ni Sanaa Ya Saikolojia Ya kukandamiza Wanyonge

 "CCTV Footage showing how the frama involving stolen car and witch doctors was stage managed". BY Mombasa County Government Watch's Video. Obtained online

Katika zama hizi za #Uwazi, #Ukweli, #Teknolojia na #Globalization, ni vigumu kuficha vitu vya kupotosha na nia ya kuua roho. Kwa kunukuu hii video clip hapa na utafiti kutoka kwenye mengine, mengi kuhusu #Ushirikina ni ya #Uongo na upotoshaji. Ukisikia Mtu anamtangazia mwenzie kuwa #Mchawi, mtu huyo mwenyewe ndie #MCHAWIMKUU.  Hakuna #Ushahidi wala uthibitisho wa #Kisheria ao #Kisayansi.

Biblia takatifu yatuambia kuwa, Mtu mwongo, Msengenyaji, Mpotoshaji, ndie mchawi na aua roho. Uchawi ni #sanaa na #imani (Mfano Dini ya Wicca) ya kupotosha na kukandamiza wengine kwenye jamii, inayotumiwa na watu wenye nia ya kuangamiza roho kwa kuathiri mtu mwingine kisaikolojia. Uchawi hauna lolote zaidi ya upotoshaji wa mtu/watu kwenye jamii na kuzua chuki za kukithiri.

Pia, Biblia Takatifu imewafananisha WACHAWI/Washirikina na watu hawa: "wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote", UFUNUO 21:8; na tena "uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo", WAGALATIA 5:19-21.

Usiwakosoe, Biblia katika kitabu cha Mithali 9:8-9 yasema hivi: "Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. 9 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu".

Mungu azidi kutubariki wanadamu na vituko vyetu. Go Figure!  🕆📖🕇✡

Utafiti/Research By Mr. Masao

Nukuu zaidi: The Definition of Witchcraft In The Bible – And Should We Be Worried About It? Link: https://www.scriptureincontext.com/the-definition-of-witchcraft-in-the-bible-and-should-we-be-worried-about-it/


No comments:

Post a Comment

Thank you for visiting us🙏🏽. Feel free, be happy, do good/right things & remember that sky is not the limit, but your eyes, dogma & imagination/mind are the only limit. My father, Sr. used to say that the mind is the most powerful resource/thing a human being can ever have; use it wisely. It is similar to a common saying that the mind is a terrible thing to waste.