Biblia takatifu yatuambia kuwa, Mtu mwongo, Msengenyaji, Mpotoshaji, ndie mchawi na aua roho. Uchawi ni #sanaa na #imani (Mfano Dini ya Wicca) ya kupotosha na kukandamiza wengine kwenye jamii, inayotumiwa na watu wenye nia ya kuangamiza roho kwa kuathiri mtu mwingine kisaikolojia. Uchawi hauna lolote zaidi ya upotoshaji wa mtu/watu kwenye jamii na kuzua chuki za kukithiri.
Pia, Biblia Takatifu imewafananisha WACHAWI/Washirikina na watu hawa: "wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote", UFUNUO 21:8; na tena "uasherati, uchafu, ufisadi, 20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo", WAGALATIA 5:19-21.
Usiwakosoe, Biblia katika kitabu cha Mithali 9:8-9 yasema hivi: "Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda. 9 Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu".
Mungu azidi kutubariki wanadamu na vituko vyetu. Go Figure! 🕆📖🕇✡
Utafiti/Research By Mr. Masao
Nukuu zaidi: The Definition of Witchcraft In The Bible – And Should We Be Worried About It? Link: https://www.scriptureincontext.com/the-definition-of-witchcraft-in-the-bible-and-should-we-be-worried-about-it/
No comments:
Post a Comment
Thank you for visiting us🙏🏽. Feel free, be happy, do good/right things & remember that sky is not the limit, but your eyes, dogma & imagination/mind are the only limit. My father, Sr. used to say that the mind is the most powerful resource/thing a human being can ever have; use it wisely. It is similar to a common saying that the mind is a terrible thing to waste.