Monday, September 20, 2021

Saikolojia Ya Jamii: Jamani Jamii Yetu Ya Mnini, Uru East, Moshi, Kilimanjaro, Utu Umetutoka

Mauaji ya Kikatili Katika Kijiji Chetu cha Mnini, Uru-East, Moshi Kilimanjaro, Tanzania. Habari kwa Mujibu wa "Global TV Online." Inasikitisha.

Hii ni mbaya sana. Jamii ya #Mnini, #UruEast, #Moshi, #Kilimanjaro, Utu umetutoka kiasi kikubwa sana. *Mungu awaongoze hawa ndugu na awafariji wafiwa.* Jamii ya Mnini imrudie Mungu, iikamate #Adabu, ijenge tabaka la kusimamia #Ukweli, irudie misingi ya #Haki.

Inasemekana hili ni tukio la 3 la Mauaji Kijijini kwetu Mnini. Ni kweli? Matukio ya Kutuchomea nyumba Moto mara mbili kutaka kunwulia Mama yetu Mjane Felicia Moshi, na usimamizi wa kubambikia makesi kila kukicha, hizi nguvu hasi zilizo chochewa na kuvumiliwa na baadhi ya watu/ndugu wanaojulika, tulivyoonya awali, hazidhuru tuu Familia ya Mwl. Valerian na Mwl. Felicia jamani. Uovu na uhalifu, nguvu hasi kwenye jamii, hazina mipaka, rangi, dini, utaufa, tabaka wala kabila.

Pole wafiwa na WanaKijiji cha Mnini. Jamani #Uvunjifu wa utu, na haki za kibinadamu Mnini ni swala linalosikitisha😩 sana. Watu wangu wa #Mnini, pazeni sauti dhidi ya uvunjifu wa utu na haki za binadamu. Usalama wetu ni jukumu letu sote. Hakuna atakaye kuja kutusaidia kurejesha Amani, utu na haki zetu, bila sisi kuanza jitihada leo hii.  

Saikolojia ya watu na jamii inatufundisha kuwa jamii ikifumbia macho matendo ya kutokuwa na adabu, utu, haki na ukweli (Uhalifu) wa kuvunja haki za bibadamu, matokeo yake ni makubwa sana. Jamii ya namna hiyo huzorota kiasi kikubwa sana, na huleta maovu mengi kwa wanajamii. 

Mfano, viongozi na raia Waliomfumbia macho Hitler, Wahutu, Iddi Amin, Kibwetere, *et la,* walichangia mauaji yaliyotokana na viongozi hawa na wapambe wao. Uchochezi/Violent Incitement ni kitu kibaya sana kwenye jamii yeyote ile. Vionhozi, iwe ni wa familia, Ukoo na Jamii, wakifumbia macho matendo ya uchochezi na kushamiri, matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu hushamiri. Tuamkeni.

Uovu/mauaji hayashamiri bila kudhibitiwa vikali ipasavyo kwenye jamii inayo jenga utu, adabu, kua wakweli na watenda haki. Kwani waovu/wauaji hawapendi mazingira ya adabu, ukweli au haki. Hawapendi kuwajibishwa, ukweli au kutiwa hatiani. 

Misingi ya usalama, adabu, ukweli na haki katika jamii ni jukumu la kila mwanajamii. Ila #Uongozi unaovunja hii misingi bayana na kuleta mgawanyiko #Ukivumiliwa, basi na uovu dhidi ya Utu utashamiri. 

Wanajamii wapenda utu na haki wakipaza sauti na kupinga uhalifu, hautashamiri. Tuambizane kila mmoja wetu, "tuanze kuilinda jamii yetu." Kwani maendeleo, huzuni, na fura ya mmoja wetu ni yetu sote. Jamani, hatuishi kila mtu kwenye kisiwa chake. 

Baba Wa Taifa alionya kuwa tukianza kubaguana/Ukabila (kukosa #Utu) ni sawa na Kula nyama ya Mwadamu, tutaendelea bila kikokomo na tabia hiyo itatapakaa kwenye jamii nzima🤔. Tutafikia malengo tuu. God help 🆘 us🙏. Go Figure!  


VPELP Reader(s) Signature and Disclaimer: Content of this Blog (ttps://vpelp.blogspot.com) is a “Me Too To retired and widow Mwalimu Felicia H. Moshi” and family, to her oppressors. The content of this blog is protected under the privacy, US First Amendment, and private property laws. Also, the contents of this Blog are mixed opinions/interpretations, views, perceptions, overreactions, experiences, and feelings by members of Valerian and Felicia Masao’s privileged real-time and real events of their private Family facts, presented by the Blogger(s). Please help us to raise awareness for the VULNERABLE people. "In God We Trust," and "United We Stand.". Contents of this Blog are intended for reading use only and not permitted for any commercial, publicity, or malicious acts. Reader(s) discretion is of the essence. Do not misrepresent, distribute, print, download, and or copy the content of this Blog without the Blog Administrator’s permission or proper academic and legal references. If you have received this link in error, please close the window and inform us promptly. Thank you, and may God bless you.

No comments:

Post a Comment

Thank you for visiting us🙏🏽. Feel free, be happy, do good/right things & remember that sky is not the limit, but your eyes, dogma & imagination/mind are the only limit. My father, Sr. used to say that the mind is the most powerful resource/thing a human being can ever have; use it wisely. It is similar to a common saying that the mind is a terrible thing to waste.